"Nasa", "Makob" na "Choli"
Hakika ameyachukua(nasa) masikitiko(makob) yetu, Amejitwika huzuni (choli) zetu; (Isaya 53:4).
NASA
Neno hili nasa kwa Kiebrania ni kuinua kwa namna ya kupeleka mbali. Neno hili limetumika kwa mbuzi aliyebeba dhambi na kuzipeleka nje ya marago wakati wa agano la lake, "Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu; naye atamwacha mbuzi jangwani" (Mambo ya Walawi 16:22). Katika Mathayo imeandikwa, "ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu."(Mathayo 8:17).
MAKOB
Masikitiko katika andiko hili tafsiri yake sahihi ni magonjwa kwa Kiebrania, inaitwa "makob".
CHOLI
Huzuni katika andiko hili tafsiri yake sahihi ni maumivu kwa Kiebrania "Choli".
Kwa huyo Isaya 53:4, inasema hakika ameyachukua na kuyapeleka mbali nasi magonjwa yetu, amejitwika maumivu yetu.
YESU AMECHUKUA NA KUPELEKA MBALI NAWE MAUMIVU NA MAGONJWA YAKO YOTE. SI MAUMIVU YAKIMWILI TU, BALI PIA HALI YOYOTE INAYOKUUMIZA, MAANA ANDIKO HALIJAWEKA MPAKA NI MAUMIVU GANI. PIA SI MAGONJWA TU, BALI PIA DHAMBI NA LAANA. MAANA MSALABANI ALITOLEWA NJE YA MJI KWA MFANO WA YULE MBUZI ILI ABEBE MATATIZO YAKO NA KUYAWEKA MBALI NAWE(WAEBRANIA 13:11-13, WAGALATIA 3:13). ANZA KUFIKIRI HIVYO NA KUSEMA HIVYO, KINYUME NA HALI ULIZONAZO, MUUJIZA UTAANZA KUDHIHIRIKA.
No comments:
Post a Comment