Wednesday, October 8, 2014

Mlango katika Jaribu

UAMINIFU WA BWANA
"Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu, Ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili." (1Wakorintho 10:13).
MLANGO UPO KATIKA JARIBU UPITIALO, UPO KWA UAMINIFU WA BWANA
1. Mlango ulkuwa bahari ya Shamu, Israeli walipofuatwa na Wamisri. Katika jaribu mlango ulitokea bahari ikafunguka.
2.Walipokuwa jangwani jaribu la maji na chakula likawepo. Hapohapo katika jaribu Mungu akashusha mana na akawapa nyama!
3.Walipatwa na jaribu la nyoka wa moto waliowauma na kuwauwa, hapohapo nyoka wa shaba akatokea walipomwangalia wakapona.
4.Goliati aliposimama mbele za Izraeli na kuwatishia, hapo hapo Daudi akatokea na kumwangusha kwa jina la Bwana.
5.Shadrak, Meshak na Abednego walipotupwa katika moto, hapo hapo akatokea mmoja wa Mbinguni kuwaokoa!
6. Daniel alipotupwa kwenye tundu la simba hapo hapo malaika akaja kumwokoa.
7.Petro alipofungwa na kanisa likaomba kwa juhudi, hapo hapo malaika akaja kumwokoa.
8.Paulo na Sila walipofungwa, wakaimba na kuomba hapo hapo milango ikafunguka.
9. Ibrahimu alipotaka kumchinja Isaka, kondoo alitokea hapo hapo katika kichaka!
MLANGO WA KUTOKEA UPO HAPO HAPO KATIKA JARIBU LAKO. JARIBU LA MSALABA LA YESU NDIO ULIKUWA MLANGO WAKE WA KUKETI MKONO WA KUUME JUU YA KILA JINA. WAKATI WA JARIBU NI WAKATI WA NYIMBO ZA SIFA, SHUKRANI NA MAOMBI, MLANGO UPO HAPO HAPO! Liambie jaribu, "Sikuogopi kwa uaminifu wa Bwana, natokea hapo hapo ulipo!"

No comments:

Post a Comment