Friday, October 10, 2014

Amefanyika Kwetu

SIYO SISI NI YESU NDANI YETU
"bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo nguvu ya Mungu na hekima ya Mungu.....Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu na ukombozi;" (1 Wakorintho 1:24,30).

NEEMA YA YESU INAONEKANA KWA MAMBO ALIYOFANYIKA KWAAJILI YETU. YATUPASA KUYASEMA NA KUYADAI KWA KUWA ALIFANYIKA HAYO ILI SISI TUWE HAYO KATIKA YEYE.

1. NGUVU YA MUNGU
Yesu amefanyika nguvu ya Mungu maishani mwetu. Nguvu yetu ni Yesu. Tuna nguvu kwa njia ya Yesu.

2.HEKIMA YA MUNGU
Ndani yetu Yesu ni hekima ya Mungu, mafumbo yote katika maisha, Kristo ndani yetu anafumbua. Hali zote zisizo na mlango yeye ni Hekima itoayo mlango.

3.HAKI YA MUNGU
Yesu ni haki ya Mungu kwetu. Sisi hatuwezi simama mbele ya Mungu. Kwasababu ya Yesu mwenye haki aliye ndani yetu, sisi pia tuna haki mbele za Mungu bila kosa! Tunasimama mbele yake pasipo hatia.

4.UKOMBOZI WA MUNGU
Yesu ni malipo ya kununuliwa kwetu. Tulikuwa watumwa wa dhambi, Sasa si watumwa tena, ametununua au ametukomboa kwa kufanyika dhambi zetu. Tulikuwa chini ya laana, ametukomboa kwa kufanywa laana msalabani. Tulikuwa wagonjwa ametukomboa kwa kupigwa kwake, tulikuwa maskini akafanyika umaskini wetu. Tulikuwa hatuna amani kwa makosa yetu, Yeye aliadhibiwa ili tupate amani.

5.UTAKATIFU WA MUNGU
Yesu ni utakatifu wako mbele za Mungu.
Wewe ni mtakatifu si kwa nafsi yako, Bali kwa Kristo ndani yako. Utakatifu wako ni Yesu, mfuate na kumtii tu, hutahangaika kuona utakatifu wake.

HAYA YOTE YESU AMEFANYIKA KWAAJILI YAKO. MUNGU ANAPOKUTAZAMA ANAMWONA YESU NDANI YAKO ALIYEFANYIKA HAYA, HAKUONI WEWE,IKIWA UMEMWAMINI YESU. USIJITAZAME WEWE, MTAZAME YESU NDANI YAKO.

No comments:

Post a Comment