Asubui hii nimehimizwa na moyo wangu kusisitiza watu wa Mungu kufanya upya ratiba zao za kusoma Neno kwa nidhamu, maisha yote. Usitafute muda kulisoma, tengeneza muda.
Unaweza kufanya zoezi la kusoma Neno kwa siku ishirini na moja mfululizo, ikiwa unataka kujenga tabia ya kusoma Neno. Wataalamu wa tabia husema, kitu kikifanywa mfululizo kwa siku ishirini na moja chaweza kuwa tabia.
Ukitata kuvunja tabia ya kutosoma Neno na kujenga ya kusoma, zitenge siku 21 zijazo kwaajili ya Neno kisha endelea.
BAADHI YA MAMBO NENO LINALOTUFANYIA
1.Ujuzi wa kweli iletayo utauwa (Tito 1:1)
*Neno linatupa ujuzi wa kiroho, ambao unatuwezesha kuwa na uungu, au utauwa.
2.Washirika wa tabia ya kiungu kwa ahadi (2petro 1:4).
*Neno linatushirikisha asili ya Mungu, linamfanya Mungu atokee kitabia ndani yetu.
*Kisha kuiondoa dunia na tamaa ndani yetu.
3.Tunapokea neno kwa upole liwezalo kuziokoa roho/nafsi zetu (Yakobo 1:21)
*Tunapolipokea neno kwa unyenyekevu na heshima, linaziokoa nafsi zetu na hali ya dunia na tamaa, Linatutakasa.
4. Neno laadibisha katika haki (2Timoteo 3:16-17).
*Neno linatufunza kutenda haki. Linatuambukiza haki, na usafi wa Mungu.
5.Neno linajenga na kutupa urithi (Matendo 20:32).
*Neno linatujenga kisha hutuwezesha kuishi kwa urithi wetu tuliopewa kwa kazi ya Yesu msalabani.
WEKA MAAZIMIO MAPYA KUANZA KULIPENDA NENO LA MUNGU. LINI ILIKUWA MWISHO WAKO KUSOMA BIBLIA. INAONEKANA WENGI SASA WAMEACHA KUISOMA. UTAINGIAJE MBINGUNI? MAANA YAKUPASA USHIRIKI TABIA YA MUNGU KWA NENO. UTASHINDANAJE NA SHETANI? UTASHINDAJE TAMAA YA MWILI? ANZA UPYA LEO, SOMA ANGALAU MILANGO MITATU KWA SIKU. SOMA KWA MFULULIZO. ANZIA INJILI YA MATHAYO MPAKA UFUNUO, KISHA RUDIA AGANO JIPYA. ANDIKA MISTARI INAYOKUPA UFAHAMU AU CHANGAMOTO, KISHA ITAFAKARI, ANZA SASA! INAWEZEKANA NI ROHO WA MUNGU ANASEMA NAWE.
No comments:
Post a Comment