Monday, September 22, 2014

NYUMBANI, MAKAO, MAHALI

Oikia, Mone, Topos
Kuna maneno mazuri yanayoonyesha moyo wa Yesu ulivyo mzuri ni haya, "Nyumbani mwa Baba yangu mna makao  mengi; Kama sivyo ningaliwaambia, maana naenda kuwaandalia mahali" (Yohana 14:2).

OIKIA
Katika andiko hili neno nyumbani kwa Baba limetafsiriwa likimaanisha mbinguni. Hapa Yesu alisema "mbinguni kwa Baba kuna makao mengi."

MONE
Makao ni neno lililotafsiriwa kutoka neno la Kiyunani "mone" likiwa na maana ya sehemu ya kuishi kama vile nyumba au majumba ya thamani. Kwa hiyo Yesu alisema, "mbinguni kwa Baba kuna nyumba, majumba mengi ya thamani ya kuishi."

TOPOS
Katika andiko hili Yesu pia amesema ameenda kutuandalia mahali. Mahali ni" topos", ikiwa na maana inayofanana na MJI.

Kwa ujumla Yesu katika andiko hili alikuwa anasema hivi, "Mbinguni kwa Baba yangu kuna majumba mengi ya thamani, maana naenda kuwaandalia mji"  Msitari wa 3 unasema, "Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali (Mji), nitakuja tena niwakaribishe kwangu, ili mimi nilipo nanyi mwepo"

        MIMI NILIPO NANYI MWEPO
Maneno haya aliyosema Yesu," Yeye alipo nasi tuwepo" Yanaonyesha nia ya Yesu ilivyo, moyoni mwake anatuwazia nini. Anataka alipo, nyumbani kwa Baba kwenye majumba mengi ya thamani katika mji wa Yerusalemu tuwepo na yeye. Anasema atakuja kutuchukua kutukaribisha kwake! Maandiko haya yanaonyesha; anatupenda, anatujali, anatufikiria vizuri, bila shaka anatuombea ili alipo na sisi tuwepo.

LEO FAHAMU YA KWAMBA UNAHITAJIKA MBINGUNI, YESU ANAYO SHAUKU NA BILA SHAKA ANAKUOMBEA AKUONE HUKO, UKIENDELEA MISTARI YA MBELE ANASEMA YEYE NDIYE NJIA YA KWENDA HUKO. AMEENDA KUTUANDALIA MAKAO, LAKINI JAMBO LA KUFURAHISHA NI KWAMBA, TUNAYAENDEA MAKAO HAYO KWA NJIA YAKE. UNAENDA MBINGUNI? NENDA KWA KUMWAMBIA YESU AINGIE NDANI YAKO. USIKOSE NYUMBANI, MAKAO NA MAHALI ALIPO YESU.

No comments:

Post a Comment