PERIERGAZOMAI
Maana ya Neno hili kwa Kiyunani ni kujishughulisha na mambo yasiyo ya maana. Kufanya vitu ambavyo isingepaswa kufanya.
Maana nyingine ni kujishighulisha na mambo yasiyokuhusu. Kufuatilia mambo ya mtu binafsi, bila sababu.
"Maana twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine" (2 Wathesalonike 3:11).
Kipengele kinachosema, "...wanajishughulisha na mambo ya wengine" kwa Kiyunani ni PERIERGAZOMAI, maana yake ni kama hizo tulizozitaja hapo juu. Hali hii kuwa ndani ya moyo wa mtu huleta dhambi, sio vizuri kutaka kujua mambo ya watu, Hata kama huna sababu ya kujua.
LEO MWOMBE MUNGU AKUPE MOYO WA KUTOTAKA KUJUA KUTAFITI MAMBO YA WATU. USIPENDE KUJUA VITU VYA WATU BILA SABABU, NI DALILI YA MZIZI WA WIVU AU USENGENYAJII.
No comments:
Post a Comment