ANOMIA
ANOMIA ni dhambi ambayo pia maana yake imebebwa na kuvunja sheria ya Mungu makusudi. Neno "iniquity" limetumika katika lugha ya Kingereza likiwa na maana ya ANOMIA kwa Kiyunani. Hii ni dhambi ambayo mtu anaifanya kwa kutafakari makusudi na kuendelea kuifanya.
Daudi alipofanya dhambi na Bashsheba, iliyopelekea mume wake kuuwawa, ilikuwa ni dhambi ya namna hii. Ni kitu alikifikiria moyoni na kukipanga kukitekeleza. Yuda Pia alimsaliti Yesu kwa jinsi hii. Alifikiri moyoni na kuendelea kutenda kosa kwa kupanga (2 Samweli 11:3–4; 2 Samweli 12:9, Mathayo 26:47-50).
Dawa ya dhambi zote tulizojifunza katika mfululizo huu ni Yesu. Imani zetu tunapoziweka kwa Yesu, tunapomtegemea Yesu, dhambi haitashinda, Yesu alisema, "Kwa habari ya dhambi, kwasababu hawaniamini mimi;..." (Yohana 16:9). Andiko hili laonyesha suluhisho la dhambi ni kumwamini au kumtegemea Yesu. Tito 2:14 inasema, "ambaye alijitoa nafsi yake kwaajili yetu, ili atukomboe na maasi yote,..." Andiko lingine lasema,"Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi na dhambi haimo ndani yake." (1Yohana 3:5). Maandiko pia yanaonyesha kwa kuwa anatupenda ametuosha kwa damu yake, "Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake." (Ufunuo 1:6).
ANZA KUMFIKIRIA YESU NA KAZI YAKE YA MSALABA. IWEKE IMANI YAKO KWAKE UNAPOITAZAMA DHAMBI INAYOKUJARIBU. HUWEZI KUSHINDA DHAMBI BILA YESU KRISTO, MWAMBIE HIVYO. PITIA SURA ZOTE SABA ZA DHAMBI TULIZOPITIA NA KUONA KAMA KUNA NAMNA FULANI UMEKOSEA. KISHA MWITE YESU AKUSAIDIE.
No comments:
Post a Comment