Kushindana na Shetani
Maana ya jina Shetani
ni adui, au mpinzani. Baalam alipopingwa
na malaika (Hesabu 22:22), malaika yule alifanya kazi kama Shetani (ingawa
hakuwa Shetani, ila kupinga huku ni kama afanyavyo Shetani). Shetani ni adui anayepinga. Anapinga Uungu usionekane. Maahali popote palipo pema atapapinga na
kuleta ubaya. Palipo na nuru atapinga na kuleta giza. Palipo na kweli atapinga
nakuleta uongo, palipo na uzima atapinga na kuleta mauti. Maandiko yanasema Mungu alimwondokeshea
Sulemani adui mwingine aitwaye Rezoni (1 Wafalme 11:23). Adui huyu alimpinga Sulemani, kama Shetani
afanyavyo. Roho ya mpinga Kristo (1Yohana
4:3), ni roho ya Shetani, inapingana na Mungu na uungu duniani (2 Wathesalonike
2:3-4).
Yesu alishamshinda
Shetani kwaajili yetu (1Wakorintho 15:57). Amemshinda na ametupa kushinda
kwake. Kumshinda Shetani huku ni kushinda ushetani, yaani upingamizi wake. Hata
hivyo Adui amebaki na kitu kimoja kinaitwa HILA. Kwa Kiyunani hila ni methodaeias, tafsiri yake ni mbinu za
kulaghai na kutega mitego. Silaha
tunazivaa ili kupinga hila na sio nguvu za Shetani, Shetani nguvu hana kwa
njia ya Yesu. Yesu alimharibu kabisa msalabani! Hatupigani naye, Yesu
alishapigana naye akamshinda. Sasa
tunashindania ushindi wake, tunahakikisha unasimama wakati wote, hatuutafuti
tunao, tunashindana usimame wakati wote.
YESU AMESHASHINDA TUNAUSHINDANIA
USHINDI WAKE
Kanunu za Kushindania Ushindi
1.Kutii na Kupinga : Yakobo 4:7-8, 1Petro 5:7-9
Wakati wote kaa chini ya mamlaka ya Yesu. Tenda asemayo, ishi kwa upendo,
Kwa kufanya hivi mamlaka yake itadhihirika kwako ukimpinga Shetani, atakimbia.
Ukipinga upingamizi wake atakimbia.
2.Kufahamu uwanja wa Mapambano: 2Wakorintho 11:3, 2Wakorintho 10:3-4
Kanuni moja ya vita ni kujua adui anapigania wapi. Shetani hupingana nasi
kwa kupitia mawazo na fikra zetu. Hulenga mfumo wa mawazo. Ukiweza kumshinda
katika mawazo yako hataweza kukupata. Akikupata mawazo yako amekupata maisha
yako. Mpinge katika mawazo kwa kusema kitu kwa kinywa, si kwa kuwaza neno tu,
bali kwa kulisema. Usemapo neno kinywani linashinda mawazoni.
3.Kufahamu Silaha Yako: Waefeso 6:17
Maandiko yameonyesha silaha kadhaa, silaha zote zinamsingi wa Neno la
Mungu. Kama vile meli inavyotegemea nanga, wakati wa mawimbi, Neno lisiache
kutoka kinywani mwako, wakati wa misukosuko tu, linashinda tu. Luka 4:1 -11, inaonyesha
Yesu alidumu kusema Neno la Mungu, Shetani alipokuwa akimjaribu au kumpinga.
Alidumu na Neno kinywani mpaka Ibilisi akamwacha, kisha malaika wakamuudumia. Udumupo
kusema neno mpinzani atakuacha mbinguni watakuudumia.
4. Walio
Upande Wako: Warumi 8:31, Zaburi 118:7
Katika mawazo yako mwone Mungu yuko upande wako, Shetani anayekuchukia
ameshindwa (Zaburi 118:7). Malaika walio
upande wako ni wengi kuliko mashetani. Kanisa la Yesu au waliookoka wako upande
wako, wana mamlaka kubwa kuliko Shetani.
Yesu aliye ndani yako ni mkuu kuliko Shetani!
5. Kufahamu Nafasi Yako: Waefeso 2:5-6
Yesu yupo juu ya kila kitu (Waefeso 1:19-23), Upo juu ya kila kitu pamoja
naye (Waefeso 2:5-6). Mashetani wote na hila zao zipo chini ya kinywa chako,
Yaani neno usemalo.
6.
Kukaa katika Roho: Waefeso 6:18, Yohana 4:23
Unamshinda Shetani kwa kukaa katika Roho Mtakatifu. Unapokaa katika ufunuo
wa Roho katika kulijua neno, Unapodumu kuomba kwa Roho Mtakatifu, Unapoishi kwa
tunda la Roho na si matendo ya mwili. Unapomwabudu
Mungu kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Wakati wote unapokuwa na ushirika na Roho
kwa kuongea naye, ni wakati kwa kumshinda adui.
7.
Kukaa katika Agano: Yohana 10:28, Yohana 6:37
Shetani hawezi kukutoa katika agano lako na Mungu kwa njia ya Yesu. Upo mikononi mwa Yesu hakuna awezaye kukutoa
hata kwa hila, mtazame Yesu aliye ndani yako na kushinda.
AMEN, GREAT LESSON, BLESS YOU PASTOR.
ReplyDelete