Monday, June 16, 2014

Kumwondoa Nyoka



Airo

“…Watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha hakitawadhuru kabisa…”
(Marko 16:18)

Kuanzia msitari wa 15 wa andiko hili kuna ishara zimetajwa ambazo zinaambatana na jina la Yesu. Msitari huu wa kumi na nane inaonyesha kwa jina la Yesu waaminio “watashika nyoka”.  Tafsiri ya kushika, hapa kwa Kiyunani ni: kuondoa, kutoa kitu na kukipeleka mbali, pia kuua.
Wazo Kuu
Kwa hiyo twaweza kusema kwa jina la Yesu tunaweza kuondoa nyoka. Kupeleka mbali nyoka, kuua nyoka.  Shetani ni nyoka.  Kwa jina la Yesu twaweza “kumshika” yaani kumwondoa popote, kumpeleka mbali, kuua kazi zake.

Maandiko yanasema lolote tufanyalo tufanye kwa jina la Yesu (Wakolosai 3:17).

Ukimwambia Shetani “Nakushika kwa jina la Yesu toka Arusha” ni sawa na kusema, “Nakuondoa kwa jina la Yesu toka Arusha”.

Siku ya leo kabla ya kuanza kazi na kabla ya kulala ‘mshike nyoka’. Mwondoe Shetani kwa jina la Yesu; katika fikra zako, familia yako, kazi yako nk. Kwa kufanya hivyo ushindi wa Kristo utazidi kuonekana kwako.

SOMA TENA, OMBA  NA KUTAMKA MANENO HAYA KABLA YA KUANZA KAZI ASUBUHI, PIA KABLA YA KULALA TAFAKARI TAMKA NA SHIRIKISHANENI KATIKA KIKUNDI NA IBADA YA NYUMBANI.







No comments:

Post a Comment