Hana Kitu Kwangu
“Mimi
sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu wala
hana kitu kwangu”
(Yohana 14:30)
Yesu anasema hapa, mkuu wa dunia, yaani Shetani, anakuja
kwake na hana kitu kwake. Mkuu huyu anayetajwa hapa katika tafsiri ya msingi ni
mjanja, mwovu, mwenye hila na mwenye akili.
Anakuja katika nafsi ya Yesu, lakini hana kitu kwake.
Hana Kitu
Yesu anasema Shetani hana kitu kwake, kwa maana ya: Hawezi
kumshika, hawezi kushirikiana naye, hawawezi kuwa pamoja. Yesu na Shetani
hawako pamoja, Shetani hawezi kukaa na Yesu wala kumkaribia.
Yesu Yupo Ndani Yako
Mahali pengine Yesu anasema anasimama mlangoni anabisha na
mtu akisikia sauti yake ataingia na watakula wote (Ufunuo 3:20). Kula na Yesu
ni kushirikiana naye, ni kushiriki nafsi
yake na hali yake. Kushiriki nguvu iliyomfufua, upendo wake, uwezo wake,
tabia yake nk. Pia kushiriki mamlaka
yake dhidi ya Shetani, ambayo imemfanya Shetani ashindwe kukaa naye. ‘Ukristo’
yaani wokovu ni Kristo pamoja nasi ni kumshiriki Kristo ni kula pamoja naye.
Mfano wa ushirika wako na Kristo ni unaonekana kwa njia ya Mzabibu(Yesu) na tawi
(wewe), (Yohana 15:1-5). Umeshiriki nafsi ya Yesu, kutoka kwake unazaa matunda.
Umeshiriki nguvu iliyomtoa kaburini kwa hiyo unazaa matunda. Sasa wewe na Yesu ni umoja. Shetani hana kitu kwako kwa njia ya Yesu
aliye ndani yako.
SEMA: Kwa Yesu aliye
ndani yangu Shetani hana kitu kwangu. Kama alivyo sasa mbinguni niko hivyo
duniani. Ananiwakilisha mbinguni kama Kuhani na mfalme, namwakilisha duniani
kama Mfalme na Kuhani. Kwa ushuhuda huu ninashinda tena leo! (Shirikisha watu
wengine ushuhuda huu, hasa katika ibada ya nyumbani.)
AMEN MTUMISHI
ReplyDelete