Thursday, August 11, 2016

JINA LA YESU-4

Siku moja nilikuwa katika hali ya maombi, Nikasikia ndani yangu maneno ya ufahamu wa rohoni yakisema:


Unapompinga Shetani, au unapomkemea sema, "Shetani ninakuzuia usitende hili (litaje), ninakuzuia kama alivyo Yesu Kristo, acha katika jina la Yesu"


Shetani anamjua Yesu alivyo mkuu na alivyomshinda. Usemapo kama alivyo Yesu na kuamuru kwa jina la Yesu, unakuwa ukiamuru kwa mamlaka ya Yesu mwenyewe. Inakuwa ni kama Yesu mwenyewe anaamuru.


Unaweza kutaja maandiko yanayoonyesha Yesu yukoje kisha kulitaja jina lake; Kwa mfano Ufunuo 1:17-18.

No comments:

Post a Comment