Friday, March 20, 2015

Ni Bure si Rahisi

IMEMGHARIMU MUNGU DAMU

Maandiko yanasema, tumeokolewa si kwa dhahabu au fedha tutoke katika mwenendo usiofaa tulioupokea kwa baba zetu, bali kwa damu ya mwana kondoo asiye na hila, yaani damu ya Yesu (1 Petro 1:18-19).

WOKOVU NI BURE LAKINI SI RAHISI
Tumeokolewa kwa neema, tunapokea wokovu kwa neema. Ingawa ni kwa neema, lakini haujapatikana bure. Imemgharimu Mungu maisha ya Yesu Kristo, yaani damu yake ya thamani.

TIMIOS

Timios ina maana ya thamani kuu, kwa lugha ya Kiyunani. Tafsiti yake ni kitu bora na cha thamani sana! Yaani damu ya Yesu, Mungu alikitoa kitu hicho Yesu aliposulubiwa msalabani.

Unaposema umeokoka jilinde, kumbuka Wokovu ulioupokea umepokea bure, ila wokovu huo umenunuliwa kwa thamani ya kumwagika damu ya Yesu. Umenunuliwa kwa Yesu kufa kwa kumwaga damu ili wewe Uishi. USIMWACHE YESU.

No comments:

Post a Comment