I.
KUMSHUKURU NI NINI?
1. KUJALI
Luka 17:15 – 16 “Na
mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti
kuu; (16)Akaanguka kifudifudi miguuni pake,
akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.”
2. KUTUKUZA
Luka 17:17 – 19 “Yesu
akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? (18)Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila
mgeni huyu? (19)Akamwambia, Inuka,
enenda zako, imani yako imekuokoa.”
Zaburi 50:23 “Atoaye
dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza.”
3. KUTOA SADAKA YA KINYWA
“Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani.” Yona 2:9 “Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya
shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa BWANA.”
4. ISHARA YA KUMJUA MUNGU
Warumi 1:21 “kwa
sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza; kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali
walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.”
II.
KUANDAA MOYO WA SHUKRANI
1. TAFAKARI FADHILI ZAKE
v Fadhili ni vitu alivyotoa kwa rehema zake
Zaburi 106:1 – 2 “Haleluya. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni
mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele. Nani awezaye kuyanena matendo makuu
ya BWANA, Kuzihubiri sifa zake zote?”
Mfano:
a) Alikuchagua katika Kristo
b) Alikuita
c) Akakuokoa
d) Akakutia muhuri wa Roho
e) Nk.
Zaburi 111:1 – 2 “Haleluya.
Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote, Barazani pa wanyofu wa moyo na katika
mkutano. Matendo ya BWANA ni makuu, yafikiriwa sana na wapendezwao nayo.”
III.
KWA MOYO WOTE
Zaburi 103:1 – 2 “Ee
nafsi yangu, umhimidi BWANA. Naam, vyote vilivyo ndani yangu vilihimidi jina
lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake
zote.”
Mhimidi (mbariki) na vyote vilivyomo ndani yangu
vilihimidi jina lake takatifu”
…………….. Mhimidi Bwana wala usizisahau fadhili
zake……..(Do not forget his benefit”
Zaburi 111:1 – 2 “Haleluya.
Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote, Barazani pa wanyofu wa moyo na katika
mkutano. Matendo ya BWANA ni makuu, yafikiriwa sana na wapendezwao nayo.”
IV.
NAMNA YA KUSHUKURU
1. SHUKURU KWA ALIYOKWISHA FANYA: Unaweza kuanza kushukuru kwa mambo yaliyokwisha pita
aliyokufanyia katika maisha au kazi ya Yesu
msalabani.
v Alimtoa Yesu
v Alikuvuta kwa Roho ukazaliwa mara ya pili
v Alikulinda toka utoto
v Hakuacha ufe kabla hujaokoka
v Aliandaa wokovu wako toka bustani ya Edeni (Mwanzo 3:15)
2. KUSHUKURU KWA ULIYONAYO SASA: Shukuru kwaajili ya mambo yaliyopo sasa. Unapoona huna
kitu fulani tafuta hapohapo ulichonacho na kushukuru.
1. Mfano; ukiwa hujafika form four, shukuru kwa kuwa
umefika darasa la saba
2. Ikiwa huna mtoto shukuru sababu una kizazi
3. Ikiwa mguu mmoja unauma shukuru sababu wa pili hauumi
4. Ikiwa huna chakula shukuru unalo jiko
5. Utagundu vitu ulivyonavyo alivyokupa Mungu ni vingi
kuliko usivyonavyo.
6. Shukuru kwa jina la Yesu (Waefeso 5:20) “na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo
yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo”
3. SHUKURU KWA YATAKAYOTOKEA:Shukuru kwaajili ya mambo yajayo, unayotarajia kuyaona
kabla hujayaona.
1. Shukuru kwa majibu ya maombi uliyoomba, kabla
ya kuyaona.
2. Shukuru kwaajili ya ahadi Mungu alizosema na
zinaenda kutokea. Kwa mfano katika jaribu shukuru kwa kutumia ahadi ifuatayo
maishani mwako:
1Wakorintho
10:13 “Jaribu halikuwapata ninyi,
isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha
mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa
kutokea, ili mweze kustahimili.”
Katika
ushindani wa kiroho unapoona mashambulizi ya kishetani, shukuru kwa ahadi
ifuatayo: Luka 10:19 “Tazama, nimewapa
amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu
kitakachowadhuru.”
Katika
huduma na udhihirisho wa nguvu za Mungu tumia, Marko 16:15 – 20 “Akawaambia, enendeni ulimwenguni mwote,
mkaihubiri injili kwa kila kiumbe.(16)Aaminiye na
kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. (17)Na ishara hizi
zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha
mpya; (18)watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha
kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao
watapata afya. (19)Basi Bwana Yesu, baada
ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu. (20)Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda
kazi pamoja na kulithibitisha lile neon kwa ishara zilizofuatana nalo.”
SIYO AHADI HIZI TU,
BALI NA NYINGINE PIA. SHUKURU KWA AHADI KANAKWAMBA ZIMESHATIMIA MAISHANI
MWAKO
V.
FAIDA ZA SHUKRANI
1. SHUKRANI INASIMAMISHA IMANI
Imani hupokea sasa na kuyaona ndani mambo yanayotarajiwa
kuonekana nje baadaye. Shukrani ni tendo la imani linaloonyesha umeshapokea
sasa. Pasipo matendo imani haizai, shukrani ni tendo linaloizalisha imani“Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa
kutoamini bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu” Warumi 4:20
2. SHUKRANI INATAKASA
Luka 17:17 – 19 “Yesu
akajibu, akanena Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? (18) Je!
Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu? (19) Akamwambi,
Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.”1Timotheo 4:1 – 5
·
Kusafisha
·
Kutenga
Mwenye ukoma alipoenda kushukuru kwa Yesu, alitakasika
kabisa, siyo kupona tu. Tunaposhukuru kwaajili ya chakula kinatakaswa.
Kinatengwa maalum kwaajili ya utukufu wa Mungu.
3. SHUKRANI INAZIDISHA
Yohana 6:1 – 13 “Baada
ya hayo Yesu alikwenda zake ng’ambo ya Bahari ya Galilaya, nayo ndiyo ya
Tiberia.(2)Na mkutano mkuu wakamfuata, kwa sababu
waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa. (3)Naye Yesu akakwea
mlimani, akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. (4)Na Pasaka, sikukuu
ya Wayahudi, ilikuwa karibu. (5)Basi Yesu alipoinua
macho yake akaona mkutano mkuu wanakuja kwake, alimwambia Filipo, Tununue wapi
mikate, ili hawa wapate kula? (6)Na hilo alilinena
ili kumjaribu; kwa maana alijua mwenyewe atakalotenda. (7)Filipo akamjibu, Mikate ya dinari mia mbili haiwatoshi,
kila mmoja apate kidogo tu. (8)Wanafunzi wake
mmojawapo, Andrea, nduguye Simoni Petro, akamwambia, (9)Yupo hapa mtoto, yuna mikate mitano ya shayiri na samaki
wawili, lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa? (10)Yesu akasema, Waketisheni watu. Na mahali pale palikuwa na
majani tele. Basi watu waume wakaketi, wapata elfu tano jumla yao. (11)“Basi Yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia
walioketi; na kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka. (12)Nao waliposhiba, aliwaambia wanafunzi wake, Kusanyeni vipande
vilivyobaki, kisipotee cho chote. (13)
Basi
wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili, vipande vya mikate mitano ya
shayiri vilivyowabakia wale waliokula.”
Baada ya Yesu kushukuru mikate na samaki viliongezeka. Unaposhukuru kwa mambo
machache ni rahisi kuongezeka.
4. SHUKRANI INAKUOKOA NA KUNUNG’UNIKA
1Wakorintho 10:1 – 12 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu
walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; (2)wote wakabatizwa wawe wa Musa katika
wingu na katika bahari; (3)wote wakala chakula
kile kile cha roho; (4) Wote wakanywa
kinywaji kilekile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba war oho uliowafuata; na
mwamba ule ulikuwa ni Kristo. (5)Lakini wengi sana
katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. (6)Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi
tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani. (7)Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa;
kama ilivyoandikwa, watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. (8)Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya,
wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. (9)Wala tumjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu,
wakaharibiwa na nyoka. (10)Wala msinung’unike,
kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu. (11)Basi mambo hayo yote yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano,
yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. (12)Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie
asianguke.” Badala ya kunungunika
kwaajili ya mambo yanayokuhusu, shukuru. Shukkrani inaondoa manunguniko na
kukufanya uendelee kumfurahia Mungu.
5. SHUKRANI INAFUFUFA NA KUONDOA HARUFU MBAYA
Yohana 11:38 – 44“Basi
Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa na
pango, na jiwe limewekwa juu yake.
(39)Yesu akasema, liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule
aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. (40)Yesu akamwambia, mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini
utauona utukufu wa Mungu? (41)Basi wakaliondoa
lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa
umenisikia. (42)Nami nalijua ya kuwa
wewe wanisikia siku zote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria
nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. (43) Naye akiisha
kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. (44)Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na
mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akamwaambia, Mfungueni, mkamwache
aende zake.”. Baada ya Yesu kushukuru Lazaro alifufuka kwa
kuamuru. Msiba uliisha! Maiti iliyoanza kunuka ikaacha. Hali hata ikiwa
imechafuka tushukuru na kutamka mapenzi ya Mungu kwa kuamuru.
6. SHUKRANI NI MAPENZI YA MUNGU
1Wathesalonike 5:18 “shukuru
kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.”
1Yohana 5:14 “Na
huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi
yake, atusikia.”
Wakolosai 4:2 “Dumuni
sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani”. Kuomba
twaomba kwa mapenzi ya Mungu, tunaposhukuru tunafanya mapenzi ya Mungu.
7. SHUKRANI ZINAENENDA NA USAFI WA DHAMIRI
2Timotheo 1:3 “Namshukuru
Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi tungu zamani za wazee wangu, kama vile
nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu usiku na mchana.”.
Shukurani zinatunza dhamiri safi.
VI. JINSI YA
KUSHUKURU
1. Kwa kushangilia moyoni. Luka 10:21 “Saa ile ile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, Nakushukuru,
Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na
akili; umewafunulia watoto wachanga; naam, Baba kwa kuwa ndivyo
ilivyokupendeza.”
2. Shukuru kwa jina la Yesu. Waefeso 5:20 “namshukuru MunguBaba sikuzote kwa mambo
yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo”
3. Shukuru kwa maneno na kuimba
4. Shukuru kwa sadaka
VII. SHUKRANI ZA
KANISA (ONGEZEKO)
Maandiko yanaonyesha
shukrani alizoshukuru hasa Paulo. Shukrani hizi
zinaweza kuleta ongezeko katika kanisa na maisha tunapozitumia.
1. Alishukuru kwakuwa Warumi Walikuwa watenda dhambi
wakatii Neema. Warumi 6:17 – 18 “ Lakini
Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa
mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; (18) na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa
watumwa wa haki.” Unaweza sasa ukamshukuru Mungu kwaajili ya kanisa au
kwaajili yako kwamba ulikuwa mtenda dhambi lakini sasa umeitii neema.
2. Shukuru imani yao inahubiriwa dunia yote. Warumi 1:8 “Kwanza namshukuru Mungu wangu katika Yesu
Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa kuwa imani yenu inahubiriwa katika dunia nzima.”
Unaweza kushukuru kwaajili ya imani yako ya wokovu, inahubiriwa, au inaweza
kuhubiriwa duniani pote.
3. Anatushangiliza daima. 2Wakorintho 2:14 “Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza
daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa
kazi yetu.”
4. Anatutia bidii. 2Wakorintho 8:16 “Lakini ahimidiwe Mungu atiaye bidii ile ile kwa ajili yenu katika moyo
wa Tito.” Shukuru kwakuwa Mungu
anakushangiliza daima. Katika hali zote zinazotokea unashangilizwa.
5. Wanalipokea Neno linatenda kazi. 1Wathesalonike 2:13 “Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu
bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata ileneno la ujumbe la Mungu amlilolisikia
kwetu, mlilipokea si kama neon la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo
lilivyo kweli kweli, litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini.”
Shukuru kwakuwa Neno la Mungu unalolipokea linatenda kazi. Ikiwa wewe ni
muhudumu wa Neno shukuru kwa Neno unalosema kwa watu wako kwamba linatenda
kazi.
6. Mungu amewachagua tangu mwanzo wapate wokovu katika
kutakaswa na Roho. 2Wathesalonike 2:13 “
Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu
mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu,
katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli.” Shukuru kwaajili yako na
kanisa kwamba Mungu amewachaagua tangu mwanzo, mpate wokovu katika kutakaswa na
Roho.
7. Omba na kushukuru
kwa macho ya kiroho kufunguka na
kuelewa mambo ya kiroho. Waefeso 1:15 – 23 “
Kwa sababu hiyo mimi nami, tangu nilipopata habari za imani yenu katika Bwana
Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu wote, (16)siachi kutoa
shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu, (17)Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape
ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; (18)macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito
wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu
jinsi ulivyo; (19)na ubora wa ukuu wa
uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za
uweza wake; (20)aliotenda katika
Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa
roho; (21)juu sana kuliko ufalme wote, na
mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humutu,
bali katika ule ujao pia; (22)akavitia vitu vyote
chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa;
ambalo (23)ndilo mwili wake, ukamilifu wake
anayekamilika kwa vyote katika vyote.”
JENGA KANUNI HIZI
1. Usifikiri ambayo huna shukuru kwa uliyonayo
2. Angalia mambo ya milele aliyokufanyia Mungu siyo ya muda
mfupi
Ukishukuru unafanya mapenzi ya Mungu. 1Wathesalonike
5:18. “shukuru kwa kila jambo; maana hayo
ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.” (Hukosei)
3. Katika hali zote Mungu anaweza tokeza jema hivyo
shukuru. Warumi 8:28“ Nasi twajua ya kuwa
katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia
mema yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.”
No comments:
Post a Comment