UKIRI WA IMANI
I.
IMANI
NI NINI? (Waebrania 11:1), “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo…”. Kwa maneno mengine tafsiri hii inasema, “ Basi imani ni uhakika, ni hati miliki ya
vitu tunavyovitarajia vidhihirike”. Imani ni hati miliki ya moyoni, unayo
hata kama mwilini huoni ulichomiliki, lakini ndani tayari unacho na una uhakika
wa kuona udhihirisho wa kutokea kwake kwa nje.
A.
Imani ni kumiliki sasa mambo yanayoenda
kudhihirika kwa kuonekana
B.
Imani ni kupokea sasa kitu kitakachoonekena
baadaye au muda mfupi ujao.
C.
Imani ni msingi wa mambo
yatakayodhihirika (hupostasis). Bila
msingi huo hayadhiriki.
D.
Kabla ya jambo kudhihirika uhakika wa
udhihirisho wake ni neno la Mungu. Neno hili huzaa uhakika huo moyoni, huwa ni
msingi wa kudhihirisha litarajiwalo.
E.
Imani ni uhakika wa moyoni wa
unaopokea sasa na kujenga tumaini akilini la kuona udhihirisho wakati ujao.
F.
Kabla ya udhihirisho imani ya moyoni
au uhakika wa moyoni, huomba, hushukuru, husifu, hukiri mambo
yasiyokuwapo kana kwamba yametokea, hufanya sasa (Warumi 4:17-21).
II.
NAMNA
ZA UKIRI WA IMANI
Kukiri ni kukubaliana na kitu fulani
na kukisema (Amos 3:3)
A. Kumkiri
Yesu (Warumi 10:9-10)
·
Kukubaliana na Yesu alivyo na kumsema
kama alivyo
·
Kukubaliana na kazi ya Yesu
aliyoifanya na kuisema
B. Kukiri
dhambi (1Yohana 1:6-8)
·
Kukubaliana na Mungu kwamba umetenda
dhambi na kusema mbele yake.
·
Kukubali kwamba umemkosea mtu na
kusema (Yakobo 5:8)
C. Kukiri
Neno (Waebrania 13:5-6)
·
Kukubaliana na neno la Mungu
linavyosema na kusema kama linavyosema, kuwa na uhakika moyoni linaenda
kudhihirika kama lilivyosema.
·
Kukubaliana na neno na kulisema 1.
Mbele za Mungu 2. Mbele za mazingira 3. Mbele za shetani, kisha kuwa na uhakika
linatokea.
D. Kukiri
habari njema (Marko 16:15-17)
·
Yesu alisema twende ulimwenguni mwote
tukahubiri kwa kila kiumbe, kuhubiri ni kukiri neno kwa wenye dhambi na kuwa na
uhakika linaenda kutenda 1. Kuponya 2.
Kuokoa 3. Kukomboa
E. Kukiri
kazi ya Yesu
·
Kusema na kuwa na uhakika
1.
Yesu alifanya nini mbele za Mungu
kwaajili yako 2Wakorintho 5:18, Wakolosai 1:20
2.
Yesu alifanya nini mbele za Shetani
kwaajili yako Wakolosai 2:15, 1Yohana 3:8
3.
Wewe ni nani katika Kristo,
2Wakorintho 5:20
4.
Una kitu gani katika Yesu Warumi 5:17
No comments:
Post a Comment