Tuesday, July 8, 2014

Upo Salama Unaye Kuhani

Unaokolewa sasa: "Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa, wao wamjiao Mungu kwa yeye: maana yu hai siku zote ili awaombee." (Waebrania 7:25). ANDIKO HILI LAONYESHA MAMBO YAFUATAYO: 1. Yesu anaweza kuwaokoa KABISA, wamjiao Mungu kwa Yeye Yesu. 2.Yu hai siku zote ili awaombee. Siku zote anawawakilisha wamwendeao Mungu kupitia Yeye. Neno kuokolewa au kuokoka kwa Kiyunani ni: SOTERIA. Maama zake ni: A. Kutolewa katika hatari B.Kuwa salama C.Kuponywa D.Kurejeshwa Baada ya kumpa Yesu maisha yako, umeokoka toka katika dhambi. Shetani siyo Bwana wako tena. Yesu ni Bwana wako. Umewekwa salama na hukumu ya milele. Msalabani Yesu alitolewa kama sadaka akupe usalama huo. Maandiko yanasema anaweza kukuokoa kabisa! Unapomwendea Mungu kwa njia ya Yesu, unaokolewa kabisa sio nusu. Sasa hivi unao usalama kabisa ikiwa unaye Yesu. Unarejeshwa kabisa, unaponywa kabisa,unalindwa kabisa, Sema hivyo! Inawezekana hali inayokuzunguka haionyeshi hivyo, ILA ukweli ni kwamba, unaye mwombezi mbele za Baba, aliyeenda mbinguni kuwa 'balozi' wa wokovu wako. Yuko mbele za Baba kuhakikisha upo salama kabisa, umepona kabisa, unalindwa kabisa, hutapotea kabisa, una amani kabisa, una ushindi kabisa nk. Amini hayo kwa kuyasema! Waza hivyo, sema hivyo kwa kuwa iko hivyo. Sema kama Paulo, "Bwana ataniokoa na mabaya yote na kunihifadhi...". Usemapo haya yanatokea kwako. Kitu chochote unachopitia kinachoonyesha uharibifu, unaye kuhani mbinguni aliyekufa kama sadaka, sasa amesimama kama kuhani kuhakikisha kwa njia take: UNATOKA KABISA KATIKA HALI HIYO, UNAOKOLEWA SASA!

No comments:

Post a Comment