Sunday, July 6, 2014

Umilele ni Rafiki na Adui

Uko Milele!

Siku moja nilijiuliza, "milele maana yake nini?" Nilikuwa nikijiuliza swali hili mara kwa mara. Siku moja ghafla nilipata jibu moyoni mwangu lisemalo, "Unapoanza kuhesabu mchanga wa dunia siku utakapo maliza utakuwa hujamaliza hesabu ya milele!"
Niligundua maana ya milele ni kubwa kuliko akili zetu ziwezavyo kuelewa.
Maandiko yanasema:      "Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; Bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele." (Mathayo 25:46).  Kuna adhabu au mauti ya milele na furaha ya uzima wa milele.
Kila binadamu unayemjua aliyeko au aliyepita mustakbali wake umo ndani ya maandiko haya:1. Adhabu ya milele 2. Uzima wa milele. Hata wewe upo ndani ya maneno haya.
                          WENYE HAKI
Wenye haki ni kina nani? Hawa sio watu watendao mambo mazuri tu! Ni watu walio na haki ya Yesu Kristo. Haki hii inapatikana kwa kutubu dhambi kwa njia ya Yesu, kumtegemea Yesu kutoka katika dhambi, kumpa maisha Yesu awe Bwana, yaani kujiweka chini yake kwa kutamka. Kutamka kwa kinywa Mungu alimfufua toka kwa wafu. Hii ni imani katika Yesu, iwezayo kukufanya mwenye haki kwa njia ya Yesu na sio kwa matendo yako. Haki hii ya Yesu inakupa uzima wa milele, milele inakuwa rafiki.
Ukimkataa Yesu, unaye adui aitwaye milele! Unayo adhabu ya milele, yaani ziwa la Moto. Tayari umeshahukumiwa(Yohana 3:36). Kama hujampa Yesu maisha ,usifanye kitu kingine kujaribu kumpata Mungu, kama vile kwenda kanisani , kuswali na mengineyo. Mungu hayupo maishani mwako bila Yesu, umepotea milele. Sema sala hii na kukaa na Yesu uwe na rafiki aitwaye 'milele':
One day I asked myself, "what Is eternity?" I continued to think on those lines, suddenly I got this impression in my heart, "when you start counting the sand particles of all the world and finish, you will not be at the end of eternity!" I knew in my spirit eternity is dangerous and threatening without Jesus. Do you know that you will live forever, in heaven or hell? There are only two destination for the humanity WITHOUT CHRIST YOU HAVE THE ENEMY CALLED ETERNITY, YOU ARE LOST FOREVER IN HELL NOW!. REPENT, SPEAK TO GOD BY FAITH, TELL HIM THAT YOU WANT TO LEAVE YOUR SINS, AND GROTESQUE DESTINATION CALLED HELL, THEN SAY TO JESUS "JESUS COME IN MY HEART, LORD JESUS" THUS YOUR ETERNITY WILL BE YOUR FRIEND THROUGH CHRIST JESUS. DO IT NOW! YESU WEWE NI HAKI YANGU MBELE ZA MUNGU. NAKUTEGEMEA WEWE KUMWONA MUNGU. BILA WEWE SINA HAKI, KWA KUWA SINA HAKI SINA UZIMA WA MILELE. NIPO KATIKA HUKUMU. YESU INGIA NDANI YANGU, NIOSHE KWA DAMU. WEWE NI MWANA WA MUNGU, ULIKUFA NA KUFIFUKA, UNANIFANYA UPYA , NINAKUWA MTU WA MBINGUNI KWA UZIMA WA MILELE, AMINA.

No comments:

Post a Comment