TAFSIRI YA IMANI
Katika somo hili utajifunza imani ni nini na mazingira ya
utendaji wake. Litakusaidia kufungulia imani ambayo tayari unayo ikiwa umempa
Yesu maisha yako. Maandiko yanasema:
“Basi imani ni kuwa na hakika
ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya
mambo yasiyo onekana” (Waebrania
11:1)
Katika andiko hili
tunaona imani ikitafsiriwa maeneo katika mawili:
1.
Kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo
2.
Bayana ya
mambo yasiyo onekana
KUWA NA HAKIKA
Kama ilivyoandikwa, imani ni kuwa
na hakika. Tafsiri nzuri ya maneno haya ni “Imani ni kuwa na uhalisi wa
sasa”. Neno la Kiyunani lionyeshalo uhakika katika andiko hili ni hupostasis. Maana ya neno hili ni “kitu kinachowekwa chini ya kitu kingine”,
ni mfano wa msingi uliobeba kitu, kama vile nyumba. Msingi wa nyumba unaweza
ukawa hauonekani, lakini ni uhakika wa nyumba kusimama, ndiyo nyumba, ni uhalisi wa nyumba!
Neno hili hupostasis pia limetumika Waebrania 1:3 “Yeye
kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa
ya nafsi yake……” Nafsi yake Mungu haionekani, lakini ndio uhakika na
uhalisi wa sasa wa Yesu anaye onekana, Yesu ni chapa, ni mwonekano wa nje wa
Mungu asiye onekana aliye uhalisi wa Yesu anayeonekana. Uhakika wa Yesu
anayeonekana ni “nafsi yake” asiye onekana.
Imani ni uhalisi unaobeba sasa, mambo yatarajiwayo kuonekana baadaye. Unayaona kwa uhalisi sasa na
kuyashika mambo yatarajiwayo kuonekana au kudhihirika baadaye.
MAMBO YATARAJIWAYO
Haya ni mambo tunayotarajia kutokea wazi ambayo yameshikwa
na imani au yamekuwa halisi tayari ndani yetu. Hakuna msingi unao beba kitu
kinachotarajiwa kutokea ila imani. Kwa mfano mguu ukiuma na ukawa unatarajia
kuona udhihirisho wa kupona, imani ni uhalisi wa sasa ndani yako, unaokupa
hakikisho sasa kwamba unalo jambo unalo tarajia kuliona, yaani mguu kupona.
Msingi wa matarajio ya kupona mguu wako ni uhalisi wa sasa uuonao ndani yako
kuhusu uzima wa mguu.
Sehemu hii ya kwanza tumeangalia Imani inabeba au inashika mambo
unayotarajia kupokea. Inayashika kabla hayajaonekana. Kabla hujapokea jambo ambalo unatarajia
kuliona likidhihirika, imani ni uhakika au msingi wa jambo hilo litarajiwalo.
Usipojenga msingi huu usioonekana hutaliona kwa nje likionekana.
Sehemu itakayofuata tutaangali BAYANA YA YASIYOONEKANA.
Thanks Pastor, its a good lesson.
ReplyDelete