MWOKOZI NA BWANA
Apeitheo
“Amwaminiye
Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini
Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.”
(Yohana 3:36)
Neno kutomwamini Mwana hapa kwa Kiyunani ni “Apeitheo”. Mara nyingi ukishuhudia mtu na kumweleza
kuhusu Yesu karibu watu wote husema wanamwamini Yesu. Wanaamini yupo na
anawapenda nk.
Neno hili asiyemwamini lina maana ya asiyekubaliana na yeye,
asiyemtii. Kuamini kwa maana ya kumtegemea Yesu kuhesabiwa haki na kuokolewa
huambatana na utii. Imani inaendana
na utii.
Umwaminipo Yesu kama Mwokozi
ni lazima umtii kama Bwana.
Wengi wakati wa sasa humpokea Yesu kama Mwokozi wao, ila hawataki aguse maisha
yao, wanataka waishi vile vile walivyokuwa! HAPANA! Utahukumiwa usipokubali
Yesu akuongoze maisha yako kama Bwana. Wokovu ni kumwamini Yesu na kusarenda
kwake, kuwa tayari kupoteza kila kitu kwaajili ya kumtii Yeye.
“Mtumwa akasema , Bwana
hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka…” (Luka 14:22). Maneno haya
yanayoonekana hapa ni maneno yanayoonyesha Bwana anavyotakiwa kutendewa. Yanatakiwa
yale yaliyosemwa naye yafanywe mara moja! Ni mara ngapi tunasikia Yesu amesema
tusamehe, lakini hatusamehi, Mara ngapi tumesikia Yesu anasema tuhubiri injili
lakini hatufanyi hivyo! Ni mara ngapi tumesikia Yesu akisema tujifunze kwake
lakini hatufanyi hivyo. Mara ngapi tumesikia Yesu amesema imetupasa kuomba siku
zote lakini hatuombi. Hebu soma Mathayo 5,6,7 na kisha umfanye Yesu awe Bwana
wako leo kwa njia ya kutii aliyosema
hapo.
Wazo Kuu
KUOKOKA NI KUMWAMINI YESU NA KUMTII YESU, HUWEZI KUSHIKA MOJA
UKAACHA LINGINE. HUWEZI KUOKOKA NA KUISHI UNAVYOTAKA WEWE, NI ANAVYOTAKA YEYE
KWA KUWA NI BWANA WAKO.
No comments:
Post a Comment