IMANI NI NINI? (Waebrania 11:1), “Basi imani ni
kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo…”. Kwa maneno mengine tafsiri hii inasema, “ Basi
imani ni uhakika, ni hati miliki ya vitu tunavyovitarajia vidhihirike”. Imani
ni hati miliki ya moyoni, unayo hata kama mwilini huoni ulichomiliki, lakini
ndani tayari unacho na una uhakika wa kuona udhihirisho wa kutokea kwake kwa
nje. Ukiwa na hati ya nyumba unauhakika kuwa unayo nyumba hiyo hata kama
huioni.
A.
Imani ni kumiliki sasa mambo
yanayoenda kudhihirika kwa kuonekana.
B.
Imani ni kupokea sasa kitu
kitakachoonekena baadaye au muda mfupi ujao.
C.
Imani ni msingi wa mambo
yatakayodhihirika. Bila msingi huo hayadhiriki.
D.
Kabla ya jambo kudhihirika uhakika wa
udhihirisho wake ni Neno la Mungu. Neno hili huzaa uhakika huo moyoni, huwa ni
msingi wa kudhihirisha litarajiwalo.
E.
Imani
ni uhakika wa moyoni unaopokea sasa na kujenga tumaini akilini la kuona
udhihirisho wakati ujao.
F.
Kabla ya udhihirisho imani ya moyoni
au uhakika wa moyoni, huomba, hushukuru, husifu, hukiri mambo
yasiyokuwapo kana kwamba yametokea, hufanya sasa (Warumi 4:17-21).
G.
Matendo haya yaani kuomba, kushukuru,
kukiri nk ni kuamini. Imani ni jina,
imani hukaa moyoni, kuamini ni tendo hufanyika mwilini kuleta udhihirisho.
Maswali
1.
Kwa Maneno yako Mwenyewe Elezea Maana ya Imani?
2.
Kuna mahusiano gani kati ya imani, kuamini na yatarajiwayo?
3.
Utafanyaje kwenye uhitaji ulionao ili uamini na kudhihirisha yatarajiwayo?
No comments:
Post a Comment