Saturday, July 5, 2014

Imani na Kuamini

Jina na Tendo

  IMANI
Imani ni JINA (PISTIS) linaloonyesha kumwona Mungu moyoni, ametenda sasa kile alichosema. Imani ni kuelewa alichosema Mungu na kukipokea sasa moyoni. Imeandikwa, "Basi imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo." (Warumi 10:17). KUSIKIA kunakotajwa hapa ni KUELEWA (Akouo- Kiyunani). Kwa hiyo andiko hili linasema, "Basi imani chanzo chake ni kuelewa na kuelewa huja kwa neno la Kristo." Imani huja kwa ufunuo wa Mungu au Neno lake moyoni na kushika moyoni jambo ambalo halionekani.

  KUAMINI
Kuamini ni TENDO (PISTEUO). Kuamini ni kutenda tendo linaloonekana lililoshikwa na imani iliyopokea sasa jibu lisiloonekana. Tendo la kwanza la kuamini ni kusema kwa kinywa, kile ulichopokea moyoni sasa (2Wakorintho 4:13) Matendo mengine ya imani ni kuomba, kushukuru, kuamuru udhihirisho katika mazingira, kuishi kwa upendo nk.
IMANI INASHIKA MOYONI YATARAJIWAYO  KUONEKANA MWILINI. KUAMINI KUNATENDA YATARAJIWAYO KANA KWAMBA YAMESHAONEKANA. KUAMINI NDIO KUNAKO DHIHIRISHA YATARAJIWAYO SI IMANI PEKEE.
Imani Jumlisha Kuamini sawa sawa na Yatarajiwayo.

No comments:

Post a Comment