MUNGU NI MKUU
"Tazama Mungu ni mkuu,nasi hatumjui; hesabu ya miaka yake haitafutiki." (Ayubu 36:26)
Ukuu Wake
Ukuu wa Mungu unaweza kuonekana katika mambo yafuatayo:
1. Mungu Anajua Kila kitu (Waebrania 4:13)
Anajua Mawazo ya Binadamu wote!
Anajua idadi ya viumbe vyote.
Hakuna kitu hajui kitakiwacho kujulikana!
2.Anaweza Yote
Mungu Anaweza kupima vumbi la dunia katika kikapu (Isaya 40:12).
Anaweza kupima milima katika mizani (Isaya 40:12).
Anaweza yote, Hazuiliki (Ayubu 42:2).
3.Amejaa Pote (Zaburi 139:7-8)
Mungu yupo kila mahali.
Yupo Ndani ya Uumbaji Wake.
Amejaa Mbinguni na Duniani.
Maajabu Makuu
Maajabu ni kwamba tulipompa Yesu maisha, tumemshiriki Mungu katika ukuu wake (1Wakorintho 3:16, 6:19-20)
Tumekuwa watoto Wake
Tumeitwa kwa jina Lake
Tumo ndani yake naye ndani yetu
Tunamwakilisha duniani
Tunao Uzima Wake
Sisi ni urithi Wake na warithi Wake(Waefeso 1:11-12)
TUMEKUWA WAKUU NDANI YAKE, TUMWABUDU KWA NJIA YA YESU
Ushangae ukuu Wake, useme, uimbe, utafakari. Ufanyapo hayo roho yako itaanza kumwabudu. Jiulize na kutafakari, Mungu aliye mkubwa hivi! Anakaaje ndani yetu! NI AJABU
AMEN! HAKIKA MUNGU WEWE NI MKUU NA NI WAAJABU!! HAKUNA KAMA WEWE!
ReplyDelete