KAZI NYINGINE ZA ROHO MTAKATIFU
I. Roho
anatuwezesha kuomba na kutumika kwa usahihi (Warumi 8:26-28)
· Tunaomba ila
si kwa usahihi wakati wote, huu ni udhaifu. Hatuwezi kuomba kwa maneno sahihi
(articulate speech) bila Roho Mtakatifu.
·
Roho hutusaidia
udhaifu huu kwa kuwa pembeni nasi na kutupa maneno ya kuomba.
·
Si kuomba tu,
hata kuimba, kufundisha na kuhubiri. Hatujui kufanya huduma kama itupasavyo huu
ni udhaifu. Roho hutusaidia udhaifu wetu, tumtegemee.
II.
Anatia nguvu
kanisa na huduma zote hasa tano kwa karama tisa.
III.
Mungu
ametumiliki kwa njia ya Roho
·
Roho ni
uhakikisho wa wakati wote katika ulimwengu wa Roho kwamba sisi ni mali ya Mungu:
1. Ni muhuri (waefeso 4:30)
2. Arabuni (Waefeso 1:14)
·
Arabuni maana
yake ni ‘deposit’ Mungu ametupa uzima wake wa milele, kwa njia ya Yesu tutaishi
naye milele. Roho aliyendani yetu anaonyesha uhakikisho huo. Muhuri ni ishara au alama ya kumilikiwa na
Mungu. Roho nadi yetu ni alama ya kuonyesha sisi tu mali ya Mungu.
IV.
Roho
anatufundisha yote
·
Yohana 2:27,
andiko hili laonyesha ‘mafuta’ yaani Roho Mtakatifu anatufundisha mambo yote!
Si ya kiroho tu, mfano:
- Kufanya biashara
- Kusoma
- Kuomba
- Kupigana vita vya kiroho
- Kuheshimu wa zazi
- Kula vizuri
- Kufunga
- Kufanya uinjilisti
- Kulea watoto
- Kuvaa vizuri nk
·
Yeye ni Msaidizi
wa maisha yetu yote, kama alivyokuwa Yesu kwa ulimwengu. Alopokuwa duniani,
aliwaponya watu, aliwapa chakula, alienda kwenye msiba, alienda kwenye mazishi
na kufufua wafu nk.
V.
Roho na huduma
ya kuufikia ulimwengu
·
Mitume
walifanya na kuamua mambo wakiwa pamoja na Roho Mtakatifu (Matendo 15:26). Roho
Mtakatifu alikuwa kama Mwenzao aliyepembeni yao kuwasaidia. Moja ya namna ya
kufanya kazi na Roho ni kujua kwamba yupo, ni kumtambua. Baada ya hapo
kumshirikisha mambo yetu, kwa kuongea naye, atatusaidia!
·
Roho ni
shahidi kwa ulimwengu (Yohana 16:13-15)
- Anashuhudia kwa kuwaonyesha watu dhambi ya
kutomwamini Yesu.
- Wanahesabiwa
Haki kwa njia ya imani ya Yesu
- Watahukumiwa Yesu
Roho alihusika katika uinjilisti wa watumishi wafuatao, soma maandiko haya kisha elezea alihusikaje?
I.
Petro
(a) Matendo 4:5-8)
(b) Matendo 10:17-19
II.
Setano
(a) Matendo 6:8-10)
III.
Filipo
(a) Matendo 8:4-8
(b) Matendo 8:26-40
No comments:
Post a Comment