JENGA USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU
Kabla
ya kufanya huduma yoyote, ni vema kujenga ushirika na Roho Mtakatifu, yeye ni
Roho wa ushirika (2Wakorintho 13:14), (Yohana 16:13-15).
Mambo
yafuatayo yatakudaidia kujenga ushirika
na Roho Mtakatifu:
I.
Tambua yupo na
wewe wakati wote. Hata kama hujisikii.
II.
Kutana naye
kwenye Neno la Mungu. Neno ni ‘kituo cha makutano’ na Roho Mtakatifu, sema ….. “ninaposoma
neno hili, leo nipo na wewe Roho Mtakatifu” . Ongea naye kama ‘mtu’ aliye pembeni
yako anayekusikiliza.
III.
Jizoeshe
ajifunue kwako kupitia Neno la Mungu.
IV.
Onyesha huwezi,
kwa kumwambia, “Roho bila wewe siwezi” (Yohana 15:5).
V.
Jizoeshe
kuikiri nafsi na uzuri wa Yesu maishani mwako Roho atatokea. Yesu akipambwa na
kusema vizuri, Roho Mtakatifu hujidhihirisha. Sema vitu vifuatavyo vya Yesu:
·
Damu ya Yesu
·
Jina la Yesu
·
Yesu mwenyewe
VI.
Ili kudumisha
ushirika usimfanyie yafuatayo
1.
Usimzimishe (1Wathesalonike 5:19)
Chochea utendaji wake
ndani yako
Mfano
- Ukianza kunena endelea kila siku, jijenge kwa Roho
Mtakatifu kwa kunena kwa lugha.
- Ukianza kusoma Neno na kujifunza kwa Roho, fanya
kila siku
- Ukiishi kwa upendo kinyume na mwili endelea
- Ukitafakari na kufunuliwa maandiko tafakari kila
siku
- Ukiomba na kuabudu endelea
- Ukiona udhihirisho wa Roho binafsi endelea
usizimishe
- Usiache kutumia karama na vipawa vya Kiungu
ulivyonavyo
Kumzimisha Roho
hufungulia mlango wa kumuhuzunisha.
2.
Usimuhuzunishe (Isaya 63:10), (Waefeso 4:30)
Roho anahuzunishwa
kwa uasi, dhambi ni uasi. Wakati wote uwe kinyume na dhambi na matendo ya
mwili. Kumuhuzunisha Roho hufungua mlango wa kumpinga.
3.
Usimpinge (Matendo 7:51)
·
Kumpinga (antipipto) ni kukataa msukumo wake kufanya
jambo, kama vile mbuzi au punda akataavyo kutembea akiamua. Roho anapokukataza
kufanya jambo fulani, ukilazimisha maana yake unampinga. Hatua hii hufungua
mlango wa kumfanyia jeuri.
4.
Usimfanyie jeuri (enubrizo)
Kumfanyia jeuri ni
sawa na kumtukana, sio rahisi mtu afikie kiwango hiki! Lakini ukiruhusu
kumzimisha utaruhusu kumhuzunisha, baada ya kumuhuznunisha utampinga, baada ya
kumpinga utamfanyia jeuri hii ni hali mbaya kuliko zote ambayo mtu anaweza
kufikia na kuvunja ushirika na Roho Mtakatifu.
Ushirika mkubwa na
Roho unajengwa kwa KUTOMZIMISHA. Kufanya mambo ya Kimungu wakati wote: Kuomba,
kusoma Neno, kufunga, kusifu na kuabudu, kusamehe, kupenda, kukiri Neno nk. Ukiwa
katika hali hii utaweza kufanya huduma ya kuufikia ulimwengu kwa ROHO
MTAKATIFU.
No comments:
Post a Comment