Huduma ya Roho Mtakatifu
Biblia au
tuseme Yesu kabla ya kuondoka alisema atatupa Msaididzi mwingine ambaye ni Roho
Mtakatifu. Neno Msaidizi limetafsiriwa toka katika neno Parakletos kwa Kiyunani. Maana za neno hili ni (1) Msaidizi (2) Wakili (3) Mmoja aliyeitwa awe pembeni ya mwingine ili amshauri au amsaidie. Roho Mtakatifu
ni Msaidizi wetu duniani, Yesu ni Msaidizi wetu mbinguni.
(a) Roho ameitwa/amaletwa awe pembeni yetu atushauri na
atusaidie. Kazi hii naamini ataendelea nayo hata tukiwa mbinguni, kutupa
tafsiri ya mambo ya mbinguni maana atakuwa nasi milele (Yohana 14:16).
(b) Kwa sasa Roho Mtakatifu anayo kazi ndani ya
kanisa na mtu mmoja mmoja aliyeamini, Maana pasipo yeye hatuwezi lolote (Yesu alisema hivi
kabla ya kuondoka, twaweza kusema sasa pasipo Roho hatuwezi lolote, maana
alimwachia Roho nafasi yake ya kuwa Msaidizi duniani Yohana 15:5).
(c) Pasipo Roho Mtakatifu kila kitu tufanyacho ni
'mwili' na wautafutao mwili hawawezi kumpendeza Mungu (Warumi 8:7-8). Ili huduma
ziwe hai na zimpendeze Mungu lazima tumtambue Roho Mtakatifu, na tushirikiane
naye. Somo hili litatusaidia tuwe karibu na Roho katika huduma.
ZIFUATAZO NI BAADHI YA HUDUMA ZA
ROHO
ZINAZOENDELEA WAKATI WOTE
I.
Kumdhihirisha
Yesu ndani yetu “katika hili tunafahamu
ya kuwa tunakaa ndani yake naye ndani yetu kwa kuwa ametushirikisha Roho wake”
(1Yohana 4:13)
·
Tupo na Yesu
na Yesu yupo nasi, kwakuwa tunaye kwa Roho wake
Mtakatifu aliye ndani yetu.
·
Vile Yesu
alivyo sasa mkono wa kuume, tunaye kwa Roho wake ndani yetu.
II.
Kufanywa upya
na hakikisho la wokovu
Roho Mtakatifu
ametuumba upya na kutupa hakikisho moyoni ya kuwa sisi ni wana wa Mungu.
·
Tito 3:5-6)
·
Warumi 8:16
III.
Kutufundisha
na kutukumbusha Neno la Mungu
·
Roho analijua
Neno lote (1Wakorintho 2:10-11)
·
Anatukumbusha
(Yohana 14:26)
·
Anatufundisha
(Yohana16:13)
·
Anajidhihirisha
kama Roho ya hekima na ufunuo tunapoomba tuelewe Neno (Waefeso 1:15-18)
·
Kwa kuelewa
neno analotukumbusha, analotufundisha na analolifunua tunapata imani, maana
imani huja kwa kuelewa (akouo) neno la Kristo (Warumi 10:17). Kwa lugha nyingine, Anatuwezesha tuishi maana
bila imani hatutaishi.
IV.
Roho Anatufanya
mwili mmoja
·
Kwa Roho mmoja
tulibatizwa kuwa mwili mmoja (1Wakorintho 12:13)
·
Tumenyweshwa
Roho mmoja ingawa tuko tofauti (1Wakorintho 12:13)
·
Viungo ni vingi
na tofauti, mwili ni mmoja kwa Roho Mtakatifu(1Wakorintho 12:20). Kama vile
katika mwili kuna damu moja na ipo ndani ya viungo tofauti, ndivyo Roho alivyo.
Roho huyo huyo yupo ndani ya kichwa (Yesu), ni huyo huyo yupo ndani ya viungo
vingine katika mwili wake Yesu. Damu katika mwili wa mtu ni moja katika kila kiungo kilicho tofauti na chenzake. Kadhalika Roho Mtakatifu katika mwili wa Kristo ni mmoja katika viungo tofauti, anatufanya MMOJA!
MUHIMU: Ikiwa kila kiungo kitashirikiana na Roho Mtakatifu,
umoja wa Roho utatokea bila kutafutwa. Katika huduma kila mmoja akiwa chini ya
Roho, sisi kama viungo tutakuwa kitu kimoja! Iwe ni katika kumuhudumia Mungu,
sisi kwa sisi au ulimwengu. Kanisa la kwanza walifahamu uwepo wa Roho na
kuutegemea wakawa kitu kimoja, tunakuwa wamoja katika Roho Mtakatifu, si
vinginevyo.
No comments:
Post a Comment