I.
KUMSHUKURU NI NINI?
1. KUJALI
Luka 17:15 – 16 “Na
mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti
kuu; (16)Akaanguka kifudifudi miguuni pake,
akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.”
Mmoja wa wenye ukoma katika maandiko haya alijali muujiza wa uponyaji na akarudi
kumshukuru Yesu. Alipata kitu cha ziada, alitamkiwa na Yesu kitu cha ziada ambacho
wenzake hawakutamkiwa. Tunapomshukuru Mungu tunajali aliyotutendea.
2. KUTUKUZA
Luka 17:17 – 19 “Yesu
akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? (18)Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila
mgeni huyu? (19)Akamwambia, Inuka,
enenda zako, imani yako imekuokoa.”
Zaburi 50:23 “Atoaye
dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza.”. Msitari wa 18 Yesu anasema, hawakuonekana
waliorudi kumpa Mungu utukufu, msitari wa 16 unaonyesha mwenye ukoma huyu alianguka
miguuni pa Yesu na kushukuru. Kwa maneno mengine kushukuru ni kumtukuza Mungu. Tunapomshukuru
Mungu tunampa utukufu. Shukrani inatulinda kubeba utukufu. Paulo katika 1Wakorintho
14:18, angeweza kusema, “ninanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote”, lakini alisema,
“namshukuru Mungu ya kuwa nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote”. Hii bila shaka
ilionyesha ni kwa nguvu ya Mungu na si yake ndiyo maana ananena kwa lugha, kwahiyo
akampa Mungu utukufu.
3. KUTOA SADAKA YA KINYWA
“Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani.” Yona 2:9 “Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya
shukrani; Nitaziondoa nadhiri zangu. Wokovu hutoka kwa BWANA.” Shukrani mbele
za Mungu ‘inashikika’ ni sadaka au dhabihu.
4. ISHARA YA KUMJUA
Warumi 1:21 “kwa
sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza; kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali
walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.”. Baada
ya kumjua Mungu yatupasa kumpa utukufu kwa shukrani.
KUANZIA LEO JENGA TABIA YA KUSHUKURU ZAIDI. MAISHA YAKO NA MTAZAMO WAKO KUHUSU MUNGU UTABADILIKA, PIA UTAANZA KUONA KIBALI CHA NAMNA YA TOFAUTI KINATOKEA.
No comments:
Post a Comment