NAMNA YA KUSHUKURU
1. SHUKURU KWA ALIYOKWISHA FANYA: Unaweza kuanza kushukuru kwa mambo yaliyokwisha pita aliyokufanyia
katika maisha au kazi ya Yesu msalabani.
v Alimtoa Yesu
v Alikuvuta kwa Roho ukazaliwa mara ya pili
v Alikulinda toka utoto
v Hakuacha ufe kabla hujaokoka
v Aliandaa wokovu wako toka bustani ya Edeni (Mwanzo 3:15)
2. KUSHUKURU KWA ULIYONAYO SASA: Shukuru kwaajili ya mambo yaliyopo sasa. Unapoona huna
kitu fulani tafuta hapohapo ulichonacho na kushukuru.
1. Mfano; ukiwa hujafika form four, shukuru kwa kuwa
umefika darasa la saba
2. Ikiwa huna mtoto shukuru sababu una kizazi
3. Ikiwa mguu mmoja unauma shukuru sababu wa pili hauumi
4. Ikiwa huna chakula shukuru unalo jiko
5. Utagundu vitu ulivyonavyo alivyokupa Mungu ni vingi kuliko
usivyonavyo.
6. Shukuru kwa jina la Yesu (Waefeso 5:20) “na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo
yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo”
3. SHUKURU KWA YATAKAYOTOKEA:Shukuru kwaajili ya mambo yajayo, unayotarajia kuyaona kabla
hujayaona.
1. Shukuru kwa majibu ya maombi uliyoomba, kabla
ya kuyaona.
2. Shukuru kwaajili ya ahadi Mungu alizosema na zinaenda
kutokea. Kwa mfano katika jaribu shukuru kwa kutumia ahadi ifuatayo maishani mwako:
1Wakorintho
10:13 “Jaribu halikuwapata ninyi,
isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha
mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa
kutokea, ili mweze kustahimili.”
Katika
ushindani wa kiroho unapoona mashambulizi ya kishetani, shukuru kwa ahadi ifuatayo:
Luka 10:19 “Tazama, nimewapa amri ya
kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu
kitakachowadhuru.”
Katika
huduma na udhihirisho wa nguvu za Mungu tumia, Marko 16:15 – 20 “Akawaambia, enendeni ulimwenguni mwote,
mkaihubiri injili kwa kila kiumbe.(16)Aaminiye na
kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. (17)Na ishara hizi
zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha
mpya; (18)watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha
kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao
watapata afya. (19)Basi Bwana Yesu,
baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa
Mungu. (20)Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote,
Bwana akitenda kazi pamoja na kulithibitisha lile neon kwa ishara zilizofuatana
nalo.”
SIYO AHADI HIZI TU, BALI NA NYINGINE PIA. SHUKURU KWA AHADI KANAKWAMBA
ZIMESHATIMIA MAISHANI MWAKO
No comments:
Post a Comment