Friday, November 28, 2014

Tunapokea kwa Kusikia

UNAPOKEA KWA KUSIKIA
"Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya Sheria au kwa kusikia kunakotokana na imani" (Wagalatia 3:2).

"Basi yeye awapaye Roho na kufanya miujiza Kati yenu, je afanya hayo kwa matendo ya sheria,au kwa kusikia kunakotokana                                                                                                                                    kunakotokana na imani" (Wagalatia 3:5)

             KINGEREZA INASEMA
" did you receive the Holy Spirit by the works of the Law or by Hearing the message of the gospel and believe?"

"He who supplies you with the Holy Spirit does so because of your believing and trusting the message that we heard"

MAMBO YA MUHIMU KATIKA MAANDIKO HAYA
1. Tunaposikia tunaelewa
2.Tunapoelewa tunaamini
4.Tunapoamini tunatenda,yaani:
Tunasema
Tunaomba
Tunashukuru
Tunasifu,nk
5.Tunapotenda Tunaona (Hatuoni kabla ya kutenda Neno)
Tendo kubwa la imani ni kusema, imani inasema.

TUTENDE KWA KUSEMA TULIYOAMINI
1.Sema  nililoomba kwa jina la Yesu nimelipokea sasa kama ilivyoandikwa (Yohana 16:23).
2. Sema, Niwekapo mkono juu ya mgonjwa anapona sasa (Marko 16:19).
3. Sema, sifadhaiki wala kuwa na woga kwa kuwa Yesu Kristo amesema(Yohana 14:27).
4.Sema, Nauvua utu WA kale na kuvaa mpya (Waefeso 4:23-25).
5.Sema, Nitamkapo chochote kwa jina lake Yesu anakifanya( Yohana 14:13).
6.Sema, mimi ni roho, sienendi kwa kuona kwanza, naanza na kutoona (2Wakorintho 5:7).
UNAPOSIKIA UNAPOKEA, UPOKEAPO UNATENDA KWA KUSEMA.

No comments:

Post a Comment