Huduma Moja kwa Wote Wakiwa Wote
Kanisa kama mwili mmoja wa Yesu, lina huduma.
Ingawa ndani yake kuna watu wenye huduma mbalimbali. Huduma hizi zinaonekana
katika huduma tano na huduma za
masaidiano. Hata hivyo ukilitazama kanisa lote kama mwili lina huduma,
inayotendwa na lote kama mwili mmoja.
A.
Kumuhudumia Mungu
Mungu ana uhitaji
ndani yake, anataka ahudumiwe kwa sifa, shukrani na kuabudu (Matendo 13:1-3).
Katika andiko hili, waalimu na manabii walimtolea Bwana ibada na kufunga,
walimuhudumia. Sisi binafsi na kama mwili wa Kristo tuna huduma ya kumuhudumia
Mungu. Kabla ya kuhudumiana sisi kwa sisi na kuuhudumia ulimwengu ni lazima
kumuhudumia Mungu kwa sifa na shukrani.
B.
Kuhudumiana
1Wakorintho 12,
inaonyesha kanisa ni mwili. Kiungo kimoja kikiumia vyote huumia pamoja nacho.
Wajibu wa mwili mzima upo kwaajili ya kiungo kimoja. Viungo vyote vinawajibu wa
kutunza kiungo kimoja. Viungo yapasa vitunzane hii ni huduma ya sisi kwa sisi,
kwa rehema, kukarimu,usimamini, maombezi, kufanya wanafunzi, kuchungwa,
kufundishwa, kufarijiwa, kujengwa, kuonywa nk. Kumhudumia Mungu vizuri kisha kuhudumiana sisi kwa sisi, huufanya mwili uwe na nguvu ya kuuhudumia ulimwengu.
C.
Kuhudumia Ulimwengu
Kanisa zima tuna wajibu
wa kuhudumia ulimwengu. Yesu alisema, “Enendeni..." (Marko 16:15-17). Wote
yatupasa kwenda ulimwenguni huu ni wito wa kanisa. Kanisa lisiloufikia
ulimwengu limepoteza lengo (shabaha) ‘limetenda dhambi’, kutenda dhambi ni
kupoteza shabaha fulani ya kiungu. Kazi ya kanisa lote ni kuhubiri injili na
kufanya wanafunzi (wafuasi watakao kuwa kama Yesu).
Kuhubiri + kufanya wanafunzi = huduma ya kanisa kwa
dunia.
v Kuhudumia ulimwengu kwa msingi ni kuufikia kwa injili.
v Huduma zote tano na za masaidiano hatma yake moja
kuu ni mwili wote uwe na ‘afya’ ya kuweza kuufikia ulimwengu.
No comments:
Post a Comment