Mwalimu (Didaskalos)
(a) Mwalimu ni mfafanuzi.
(b) Mwalimu ni mchambuzi.
(c) Apolo alikuwa mwalimu (Matendo 18:24)
(d) Mwalimu ni huduma inayojitegemea na inaweza
kusimama kama yenyewe, ila inahitaji ushirika ili iwe na ufanisi (Matendo 13:
1-3). Andiko hili halisemi hapo Antiokia kulikuwa na wachingaji waalimu na manabii, linasema kulikuwa na waalimu na manabii. Hii inaonyesha mwalimu anaweza kuwa mwalimu bila kuwa mchungaji.
(e)Mchungaji anafundisha, lakini si lazima awe
mwalimu ili awe mchungaji. Ingawa kuna wachungaji na waalimu kwa wakati mmoja.Ni kama kuhubiri, si kila muhubiri ni mwinjilisti kwa wito, hata mchungaji anaweza kuhubiri, ingawa si lazima awe mwinjilisti.
(f) Mwalimu naye, lakini sio lazima awe
mchungaji (Matendo 13: 1-3).
(g) Kazi ya mwalimu ni kutia maji mbegu iliyokwishapandwa
na mtume au mwinjilisti(1Wakorintho 3:6). Kazi ya Mchungaji ni kusimamia mmea
ambao unakuwa; Ingawa mchungaji pia anaweza kupanda, kutia maji na kusimamia si
sheria.
(h) Walimu wenye huduma ya ualimu peke yake husafiri
kama wainjilisti au huwa katika timu za kitume (Matendo 13:1-3).
(i) Walimu ni wadadisi na hufafanua maandiko.
(j) Mwalimu ni vizuri awe tayari kufundishwa wakati wowote na kukosolewa, Akila na Prisila walimfundisha Appolo, ingawa alikuwa hodari wa maandiko, bado Appolo alikuwa hajui kila kitu (Matendo 18:24-26).
Aina za walimu
1. Anayefundisha yeyote
Mtu anapofundisha
hata kama hana huduma ya ualimu ni mwalimu kwa wakati huo. Mfano mwalimu wa
watoto, “Sunday school” nk.
2. Mtu aliyeitwa katika huduma ya ualimu na
kufundisha neno
(a) Hufundisha kwa ufahamu wa Roho
(b) Hufundisha kinabii- Neno la wakati
(c)Hufafanua maandiko kwa kutumia maandiko mengine, ili kujenga hoja na kuithibitisha.
(k) Mwalimu hufundisha kwa kujifunza kwa ufunuo wa Neno, katika Roho Mtakatifu, majaribu, na uchambuzi wa maandiko.
(l) Nyenzo za mwalimu ni: Biblia, ufunuo wa Roho Mtakatifu,
kuomba kwa Roho kwa muda (Kunena kwa lugha), Kusoma sana vitabu (2Timoteo 4:13), na nidhamu katika maisha. Mwalimu lazima awe na nidhamu ya kujifunza kwa Roho Mtakatifu na kutunza kumbukumbu maisha yote ili adumu kuwa mwalimu, hivi hivi atapwaya.
KAZI YA HUDUMA TANO(Waefeso 4:11-13)
(i) Kuwakamilisha watakatifu (wakue, wafanane na Yesu)
(ii) Kuwafanya wahudumu(watumike)
(iii)Kujenga mwili wa
Yesu kiubora na kiidadi
No comments:
Post a Comment