MATENDO 15:14
Katika Agano la kale Israeli peke yake ndiyo walikuwa watu wa Mungu, Walioitwa kwa jina lake: Yaani Mungu wa Israeli. Kwa njia ya kusikia na kuamini injili ya Yesu, Mataifa waliitwa na kuingia kuzishiriki baraka za Israeli, kama vile; Roho Mtakatifu na Imani nk (Matendo 15:7-9). Katika Waefeso 2:13, Maandiko yanasema, sisi Mataifa tulikuwa mbali, lakini sasa tupo karibu kwa damu ya Yesu. Kwa damu tuko karibu tunalishiriki jina la Mungu wa Israeli kama Waisraeli walivyolishiriki, sasa tunalishiriki kwa njia ya jina la Yesu.
Kuokolewa ni kuchaguliwa kwaajili ya jina lake Yesu. Haujampa Yesu maisha yako hivi hivi tu! Umempa na umeitwa kwaajili ya jina la Yesu. Leo fahamu ya kuwa upo kwaajili ya jina la Yesu, Hili ni jina la Mungu wa Israeli katika mwili. Kama umeajiriwa mahali unajua kabisa uliposailiwa Ilikuwa ni kwaajili ya nini, na umeingia katika kazi hiyo kwaajili ya nini.
Kadhalika katika wokovu umeokolewa kwaajili ya jina lake. Naweza kugawanya sehemu mbili:
1.Kwa ajili ya jina lake, ndio maana umebadilika na kuwa mtu aendae mbinguni, Si kwa nguvu nyingine yeyote. Ni kwa nguvu iitwayo: Jina la Yesu.
2.Kwaajili ya kulionyesha jina lake, ndio maana upo ndani ya ufalme wa Mungu. Chochote unachofanya; kama ni maisha ya kawaida, huduma kazi nk, Unafanya kwaajili ya jina lake. Ukiwa katika ufalme unakifanya kwaajili ya jina lake; Kinapotimia sifa na utukufu zinarudi kwa jina la Yesu.
MARA ZOTE JIULIZE UTALIFANYIA NINI JINA LA YESU ILI LITUKUZWE? JE UTALITUMIA? LITAKUTUMIA? ILI LITUKUZWE?
No comments:
Post a Comment